Kila la kheri wawakilishi wetu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Mar 2018
Kila la kheri wawakilishi wetu
Licha ya upinzani wa jadi baina yao, Simba na Yanga leo zinapeperusha bendera ya Tanzania katika michezo yao muhimu ya Kimataifa.

Yanga watakuwa wageni wa Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone, Botswana kuanzia Saa 10:45 jioni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa na Simba watakuwa wageni wa Al Masry Uwanja wa Port Said nchini Misri kuanzia Saa 2:30 usiku.

Yanga wanahitaji lazima ushindi wa mabao 2-0 ili kwenda hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba SC wanahitaji ushindi wowote, hata wa 1-0 ili kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mchujo baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

Yanga ikiitoa Rollers itakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ambayo kihistoria itakuwa mara yake ya pili baada ya mwaka 1998, lakini ikitolewa itaingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Simba SC ikishinda leo itacheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho, lakini ikitolewa itarejea nyumbani moja kwa moja.

Kila la heri wawakilishi wetu. Mungu zibariki Simba na Yanga. Mungu ibariki Tanzania.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’