Mabosi wa Simba wameshtukia jambo na kuamua kufanya maamuzi magumu ya kuwabadilishia wachezaji wake ratiba ya chakula cha mchana leo Ijumaa huko Misri
Mabosi hao chini ya usimamizi wa Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Tryagain' wamesitisha mchakato wa nyota wake kupata chakula cha mchana kwenye hoteli ya Nora and Style waliyoshukia kwa hofu ya kufanyiwa hujuma na wenyeji wao Al Masry.
Mabosi hao wakaagiza chakula kutoka hoteli nyingine kwa ajili ya wachezaji wake ili kukwepa fitna za wenyeji wao hao ambao wanasifika kwa kutafuta ushindi kwa njia za mkato.
Simba itacheza mchezo wake wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry Port Said, Misri kesho Jumamosi usiku hivyo mabosi hao wameanza kupata hofu ya hujuma na kuamua kufanya mambo tofauti.
Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.
Mbali na hilo, wamepiga marufuku mtu yeyote asiyekuwa Mtanzania kuingia kwenye vyumba vya wachezaji na pia kuzungumza chochote na wenyeji.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE