Hatuihofii Al Masry - Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Mar 2018
Hatuihofii Al Masry - Okwi
Mshambuliaji tegemeo na nyota katika kikosi cha Simba, Emmanuel Okwi, amesema wamekwenda Misri kupambana na hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Al Masry utakaofanyika Jumamosi kwenye mji wa Port Said.

Kikosi cha Simba tayari kimetua Port Said ambapo mchezo wao utafanyika.

Okwi, amesema kuwa anaamini Simba ina nafasi "kubwa" ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na wanachohitaji ni kuwa na bahati.

Okwi amesema kuwa uwezo wa kushinda mechi hiyo wanao lakini wanatakiwa kuongeza umakini na kutoziweka akilini "fitna" zozote za nje ya uwanja ambazo zitajitokeza kabla ya kushuka uwanjani.

"Tunakwenda kupambana, naamini Mungu atatusaidia, uwezo tunao, mliwaona, wanafungika," alisema kwa kifupi Mganda huyo.

Simba iliondoka jana jioni na msafara wa wachezaji 20 ambao ni Said Mohamed, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein "Tshabalala", Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, Paul Bukaba, Jonas Mkude na James Kotei.

Wengine ni Said Ndemla, Muzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya, John Bocco, Okwi, Nicholaus Gyan, Laudit Mavugo na Juma Luizio huku benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Pierre Lechantre, Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, Mohammed Aymen (viungo), Muharami Mohammed (makipa), Yassin Gembe (daktari), Richard Robert (meneja) na Yassin Mtambo (vifaa).

Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Machi 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, hivyo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kusonga mbele.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’