Kikosi cha Simba kikiwa na wachezaji 20 na viongozi tisa wanaondoka nchini leo jioni kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Al-Masry huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
Kocha msaidizi wa Simba amesema wachezaji wao wanafahamu kazi bado haijaisha na wanaenda Misri kwa lengo moja la kulazimisha ushindi kwenye michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.
"Bado mchezo upo wazi kwa timu zote, kwetu kazi bado haijaisha, tuaenda Misri kwa lengo moja la kulazimisha ushindi tuweze kusonga mbele," alisem Djuma.
Simba italazimika kupambana kupata ushindi au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Hiyo inafuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2 waliyoyapata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Simba, inategemea silaha zake, washambuliaji John Bocco, Shiza Kichuya, Jonas Mkude na Emmanuel Okwi kuweza kulazimisha ushindi kwenye mchezo huo utakaochezwa Jumamosi.
Kama Simba itafanikiwa kusonga mbele, itasubiri kupangiwa timu ya kucheza nayo 'Play Off' kabla ya kuinga kwenye hatua ya makundi

ADVERTISE HERE