Utulivu ndio silaha ya kuiondoa Al Masry kwao - Djuma

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Mar 2018
Utulivu ndio silaha ya kuiondoa Al Masry kwao - Djuma
Wakati ikitarajia kuondoka nchini kesho Jumatano kwenda Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema "dawa kubwa" ya kuhakikisha wanawafunga Waarabu na kusonga mbele ni utulivu.

Simba itashuka dimbani ugenini katika mji wa Port Said Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya sare ya mabao 2-2 waliyoipata katika mechi ya kwanza iliyofanyika Machi 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Djuma ambaye kwa sasa anashirikiana na kocha Mkuu Pierre Lechantre amesema kuwa wakiwa ugenini watacheza bila presha na endapo wachezaji wao watatulia na mipira, nafasi ya kuwafunga na kupata ushindi itapatikana mapema.

Djuma amesema kuwa kama hakuna utulivu na umakini, si wao wala wapinzani watakaoweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa marudiano ambao atakayeshinda atapata nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo ya kimataifa.

"Maandalizi yanakwenda vizuri na tunaamini uwezo wa kuwafunga tunao, mfumo gani tutacheza huko ni siri ya kocha mkuu, tusubiri muda na siku hiyo mtaiona timu itakavyopambana," alisema Djuma, kocha wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.

Aliongeza kuwa wanawajenga wachezaji wao kuufikiria mchezo huo wa kimataifa kwanza na kusahau vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo wanapigana na mahasimu wao Yanga.

"Hakuna mechi rahisi, hakuna mashindano rahisi, tuko vitani, tunaamini sisi si wasindikizaji, tumeingia kushindana na kupambana kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki, tunajua kiu ya Simba katika ligi na mashindano ya ndani, pamoja tuñaweza,"

Wakati huo huo uongozi wa Simba umewataka mashabiki walio tayari kuongozana na kikosi hicho ili kwenda kuwashangilia katika mechi hiyo ya marudiano itakayofanyika kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za Misri.

"Gharama ni Dola za Marekani 500 ambazo ni kwa ajili ya tiketi ya kwenda na kurudi pamoja na viza, safari itakuwa ni Ijumaa na kurudi Dar es Salaam Jumapili," alisema Haji Manara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’