Mwalimu Kashasha aipa Simba nafasi ya kutwaa ubingwa VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
12 Mar 2018
Mwalimu Kashasha aipa Simba nafasi ya kutwaa ubingwa VPL
Mchambuzi mahiri nchini, Alex Kashasha ‘Mwalimu Kashasha’ ameweka wazi kuwa Simba ina uwezekano wa mkubwa wa kuchukua ubingwa wa msimu huu kwa asilimia sitini iwapo haitofanya uzembe wa kubweteka.

Licha ya kushiriki michuano ya kimataifa, Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 46, Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 43 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 41, wote wakiwa wamecheza michezo 20 hali inayofanya ushindani wao kuwa mkubwa.

Akizungumza na Spoti Xtra , Kashasha alisema Simba wana nafasi kubwa sana lakini Yanga ikicheza karata zake inaweza kupindua meza.

“Kiukweli kwa namna Simba walivyosimama msimu huu wana asilimia sitini ya kuchukua ubingwa kutokana na mtaji mkubwa wa mabao waliokuwa nao, wakifanya uzembe wa aina yoyote au wakajiachia wakakutwa na Yanga kwa maana ya mabao itakuwa ngumu kwao. “Lakini uwezo wa wao kuchukua ubingwa kwa upana wa kikosi chao ni mkubwa ndani ya msimu huu.

Wachezaji kama wataendelea kufanya mzunguko wa kubadilishana kucheza wote kwa sababu kumekuwa na shida kwenye nchi hii kwamba timu nyingi wanasajili wachezaji 30 lakini unakuta wanaocheza ni 12, 13 au 14.

“Sasa kukitokea majeruhi ndiyo mtu sasa anaonekana kucheza kama ilivyotokea kwa Azam baada ya Razak Abalora kupata matatizo ndiyo Mwadini Ally ameanza kucheza, sasa kama watatumia vizuri wachezaji hakutakuwa na cha kuwazuia kuwa mabingwa,” alisema Kashasha ambaye mbwembwe zake za lugha kwenye uchambuzi zinawakosha mashabiki.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →