Simba yafunika kwa mapato mechi za Kimataifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Mar 2018
Simba yafunika kwa mapato mechi za Kimataifa
Klabu ya Simba imeipiku Yanga katika mapato ya mlangoni kwenye mechi za kimataifa zilizochezwa mapema wiki hii.

Yanga ilicheza na Township Rollers ya Botswana Jumanne wiki hii Machi 6 ikiwa ni mchezo wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika na kunyukwa mabao 2-1 wakati Simba ilicheza Kombe la Shirikisho na Al Masry Jumatano Machi 7, na kutoka sare ya mabao 2-2.

Mechi hizo zimefanyika kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mchezo wa Simba uliingiza mashabiki wengi zaidi ya Yanga baada ya kuingiza kitita cha Sh milioni 85 baada ya mashabiki 14, 798 kudhuria mchezo huo.

VIP A waliingia Watazamaji 250 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000, VIP B na C waliingia Watazamaji 557 kwa kiingilio cha shilingi 15,000 ikapatikana jumla ya Sh 8,355,000, majukwaa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 13,644 kwa kiingilio cha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 68,220,000

Akitoa mchanganuo wa mapato hayo, Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema Simba imepata shilingi 43, 585, 346 baada ya kukatwa VAT 12,972,966.10, Selcom 5,017,655.00, TFF 3,352,718.94 na gharama za uwanja 10,058,156.83, gharama za mchezo 6,034,894.10, BMT 670,543.79 na CAF 3,352,718.94

Kwa upande wa Yanga, Ndimbo alisema kuwa timu hiyo ya mtaa wa Jangwani ilihudhuriwa na mashabiki 9,961 na kuingiza Shilingi milioni 56,245,000 na Yanga kuambulia shilingi 28,825,419 baada ya makato mbalimbali na kwamba VIP A wameingia watazamaji 99 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 1,980,000,

VIP B na C waliingia Watazamaji 991 kwa kiingilio cha shilingi 10,000 ikapatikana jumla ya shilingi 9,910,000, majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 8,871 kwa kiingilio cha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 44,355,000.

Ndimbo akitoa mchanganuo katika mchezo huo alisema VAT 8,579,745.76 Selcom 3,318,455.00, TFF 2,217,339.96, uwanja 6,652,019.89, gharama za mchezo 3,991,211.93, BMT 443,467.99 na CAF 2,217,339.96.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’