Lechantre aongeza dozi ya mazoezi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Mar 2018
Lechantre aongeza dozi ya mazoezi Simba
Simba imepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry baada ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Njombe Mji kuahirishwa.

Kocha wa Simba Pierre Lechantre amepania kutumia muda huo kukiandaa kikosi chake kikamilifu ili kuweza kuibuka na ushindi nchini Misri.

Aidha, Lechantre ameweka hadharani mambo manne ambayo yatakwenda kuwamaliza Al Masry kule kule Misri, huku akionyesha kushangazwa na soka tamu lililopigwa na kikosi chake kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Alisema katika mechi ya kwanza, kiwango cha wachezaji wake kilikuwa kikubwa kwani walitimiza vyema maelekezo aliyowapa wakati wa mazoezi ya maandalizi kuelekea mechi hiyo.

Alisema walicheza na timu kubwa ambayo imekamilika kila idara ambayo kila timu inapaswa kuwa hivyo, lakini kikosi chake kilikuwa vizuri ingawa matokeo hayakuwa mazuri kama walivyotarajia.

"Jambo la kwanza ambalo nitalifanya kuelekea katika mechi ya marudiano ni kuongeza mazoezi ya nguvu zaidi ambayo tumewahi kuyafanya, kuwatengeneza wachezaji kisaikolojia kwani Al Masry wapo vizuri kwenye hilo na nimeshawahi kuona mambo kama haya pindi nilipokuwa nafundisha Misry.

"Kuongeza umakini katika kutumia vizuri kila nafasi tunayoitengeneza kwenye kufunga na mwisho kupunguza makosa ya kutokukaba hadi mwisho kama tulivyofanya," alisema Lechantre na kuongeza;

"Kama tukifanya mambo haya vizuri katika mechi ijayo nina imani tunaweza kupata matokeo mazuri na kosonga mbele, ingawa halitakuwa jambo rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wetu, lakini tupo tayari kukabiliana."
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’