Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, Simba imefikisha alama 76, ambazo ni Yanga tu inayoweza kuzifikia
Hata hivyo Simba imefunga mabao 29 zaidi ya Yanga, mechi mbili zikiwa zimesalia kwa upande wa Yanga wakati Simba ina michezo mitatu
Ushindi au sare kwenye mchezo ujao dhidi ya Coastal Union ni matokeo ambayo yataifanya Simba ifikishe alama ambazo hakuna timu inaweza kuzifikia
"Nawapongeza vijana wangu kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wetu. Ulikuwa msimu mrefu na hakika tumepambana kufika hapa. Nafikiri kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji ambao wamecheza muda mrefu"
"Kikosini nina wachezaji wazuri wengi lakini hawakuwa wakionekana uwanjani kutokana na ushindani wa nafasi. Wachezaji kama Said Ndemla, Miraji Athumani ni miongoni mwao," alisema Gomes
Mchezo dhidi ya Coastal Union utapigwa Jumapili Julai 11, kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Azam Fc, Jumatano Julai 14 na kumaliza msimu Julai 18 kwa mchezo dhidi ya Namungo Fc