Simba imeunguruma uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuichapa KMC mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, raundi ya 31
Mabao mawili yaliyowekwa kambani na Chris Mugalu katika dakika ya 3 na dakika ya 44 yameihakikishia Simba ushindi muhimu uliwahakikishia kuurejesha ubingwa Msimbazi kwa msimu wa nne mfululizo

Simba imefikisha alama 76 baada ya kushuka dimbani mara 31 ikiwa na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa 58
Yanga inaweza kufikisha alama 76 kama itashinda michezo yake miwili iliyobaki lakini inapaswa kufunga mabao 29 yaani kila mchezo wafunge angalau mabao 15!
Hongera kwa wachezaji wa Simba kwa kurejea wakiwa imara leo licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga
Ni ubingwa wa nne mfululizo na hakuna shaka ahadi ya kushinda mara 10 mfululizo iko pale pale...!