Droo ya mchujo wa Kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika soka la wanawake kwa ukanda Afrika Mashariki na kati ( Cecafa) inafanyika leo
Tanzania Bara itawakilishwa na mabingwa Simba Queens katika michuano inayotarajiwa kufanyika Kenya kati ya Julai 17 hadi Agosti 1
Simba Queens , Lady Doves FC (Uganda) na Benki ya Biashara ya Ethiopia FC ndio timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa na kukata tiketi moja ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika
Timu nyingine ambazo zitashiriki ni pamoja na; PVP FC (Burundi), FAD Club (Djibouti), Scandinavia WFC (Rwanda), Yei Join Stars (Sudan Kusini) na New Generations FC (Zanzibar)
Timu sita za juu (moja kutoka kila Kanda ya CAF) na mwenyeji wa mashindano ya mwisho (Misri) pamoja na timu moja ya ziada kutoka Kanda iliyoshikilia taji la Kombe la Mataifa ya Afrika la Wanawake la mwaka uliopita (2018) watafuzu kwenye mashindano ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake