Mabingwa wa nchi Simba leo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu wa Vodacom ambao ni wa kiporo
Huu ni mchezo muhimu kwa Simba ambapo matokeo ya ushindi yatawahakikishia wekundu hao wa Msimbazi kurudisha ubingwa kabatini kwa msimu wa nne mfululizo
Aidha ni mchezo ambao Simba inaweza kuutumia kurudisha furaha ya mashabiki wake baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga
Selemani Matola ambaye ni kocha msaidizi wa Machampioni hao wa soka nchini, amesema maandalizi yamekamilika huku matumaini ya ushindi yakiwa makubwa.
Simba inatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka kwa KMC lakini bila shaka vijana wa Didier Gomes wataweza kuwapa furaha mashabiki wao kwa kuibuka na ushindi
Mechi itapigwa kuanzia saa moja usiku.