Kesho Jumatano mabingwa wa nchi Simba watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ambao ni kiporo
KMC watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku
Simba inaweza kutangaza ubingwa katika mchezo huo kama itafanikiwa kuondoka na alama zote tatu
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Coastal Union, utapigwa Jumapili Julai 11 uwanja wa Benjamin Mkapa
Bila shaka katika michezo hii Simba itafunga hesabu za msimu huu kwa kulirejesha Msimbazi taji la VPL kwa msimu wa nne mfululizo
ADVERTISE HERE