Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema amezibeba lawama za kupoteza mchezo dhidi ya Yanga juzi huku akiwaahidi mashabiki kuwa waahakikisha wanapata ushindi katika mchezo unaofuata dhidi ya KMC
Gomes amesema wachezaji wake walipambana kwa kiasi kikubwa katika mchezo dhidi ya Yanga licha ya kuwa kuna mahali walifanya makosa na kuadhibiwa
"Tulipambana vizuri, hatukuwa na bahati ya kupata matokeo, ila inaumiza hasa kuona mashabiki wanapoteza furaha"
"Tutahakikisha tunaende kujipanga kwa ajili ya mechi yetu ijayo dhidi ya KMC Fc ambayo tunahitaji kupata pointi tatu ili kutangaza ubingwa," alisema Gomes
Gomes amesema katika mchezo dhidi ya Yanga walitengeneza nafasi nyingi za wazi lakini wakashindwa kuzitumia licha ya kucheza kwa kiwango bora zaidi
Mchezo dhidi ya KMC utapigwa keshokutwa Jumatano, Julai 07 uwanja wa Benjamin Mkapa