Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amewakumbusha wachezaji kuwa wanapaswa kuipa Simba thamani yake wawapo uwanjani
Manara ambaye jana alialikwa kisiwani Pemba kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Suluhu, alisema ameyaona machungu ya mashabiki wa Simba walioumizwa na matokeo ya kufungwa na Yanga juzi
Aidha Manara amesema yeye binafsi haoni sababu ya kuendelea na majukumu yake kama wachezaji hawawezi kujitoa katika mchezo utakaopigwa mkoani Kigoma Julai 25
"Nahodha John Bocco sema na wenzio, mtakuja kuua watu Kwa makundi siku moja"
"Naambiwa Dar kuna Shabiki kajinyonga sababu ya matokeo ya mchezo dhidi ya Yanga"
"Kipindi cha kwanza mmecheza kama mmelazimishwa au mnadai kitu, mmezinduka kipindi cha pili na wao wakaweka kontena mechi ikaisha"
"Wallah kigoma tukifungwa naacha hii kazi narudi shamba kulima. Viongozi wanatimiza majukumu yao,Washabiki wanajaa kuliko Washabiki wao kwa mbali mno. Mimi natukanwa kutwa Kwa kuwapa nguvu nyie lakini mmeenda kutuangusha"
"Sioni sababu ya kuendelea na kazi hii kama wachezaji hawajui nini maana ya uzito wa dabi"
"Wachezaji wao wanajitoa asilimia elfu moja toka dakika ya kwanza, sisi tunazinduka kushakuchwa. Kaeni wenyew zungumzeni na thamani ya jezi ya Simba ilindwe," aliandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii