Tutawafunga hukohuko kwao - Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Mar 2018
Tutawafunga hukohuko kwao - Okwi
Mshambuliaji tegemeo wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema kuwa hana hofu yoyote na mchezo wa ugenini wa marudiano wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry na kuongeza kuwa Waarabu hao wanafungika.

Simba itawafuata Al Masry katika mechi ya marudiano itakaofanyika Machi 17 mwaka huu katika mji wa Port Said.

Okwi, anaamini mechi hiyo ya marudiano haitakuwa ngumu kama ya juzi kwa sababu tayari wameshawafahamu wapinzani wao.

Okwi alisema kuwa anaamini benchi la ufundi litayafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mechi ya juzi na hatimaye kuwadhibiti Al Masry na kusonga mbele katika michuano hiyo inayoandaliwa kila mwaka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

"Mechi ilikuwa ngumu lakini tuliongeza bidii na kufanikiwa kusawazisha, kikubwa hatukupoteza mechi na tunao uwezo wa kuwafunga huko kwao kwa sababu hatutaenda kuzuia," alisema mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Uganda.

Naye Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma, amesema kuwa wanamshukuru Mungu hawajafungwa katika mechi ya kwanza na dunia ya sasa timu zinaweza kushinda ugenini na kusonga mbele.

"Vijana walipambana kwa nguvu kuhakikisha wanapata mabao, mpira ulikuwa mgumu katika kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili kilikuwa chetu ila umeme na mvua vilituharibia, yote ni mipango ya Mungu lakini tumelinda heshima ya kutofungwa nyumbani," alisema kocha huyo.

Simba ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara itahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kusonga mbele katika mashindano hayo na inatarajia kuanza mazoezi leo kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’