Chikwende aruhusiwa kujiunga na timu ya Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Jul 2021
Chikwende aruhusiwa kujiunga na timu ya Taifa

Kiungo mshambuliaji wa Simba Perfect Chikwende ameruhusiwa kurejea kwao Zimbabwe kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa

Michuano ya COSAFA inayohusisha Mataifa ya Kusini mwa Afrika, inatarajiwa kuanza hivi karibuni

Ni wazi Chikwende atakosa mechi zilizosalia kumaliza msimu

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema hii ni nafasi kwa Chikwende kuimarisha kiwango chake

"Ni kweli benchi la ufundi limeamua kumrudisha Chikwende Zimbabwe, kuungana na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo inayojiandaa na mashindano ya COSAFA"

"Tumefanya hivi kama sehemu ya programu maalum ya kumpa Chikwende muda mwingi zaidi wa kucheza, na kuzidi kuimarisha utimamu wake wa mwili, na bila shaka kama atazingatia programu tuliyompa basi atarejea akiwa bora zaidi," alisema Gomes

Chikwende alisajiliwa na Simba usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Fc Platinum. Alikuwa na wakati mzuri mwanzoni kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa

Baada ya kupona majeraha hayo, imekuwa ngumu kwake kuingia kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
55m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’