Julai 03 ni leo, hawatoki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jul 2021
Julai 03 ni leo, hawatoki

Waswahili wana msemo wao usemao kuwa mbio za Sakafuni huishia ukingoni! Ndivyo ilivyo kwani baada ya 'kuingia mitini' May 08 kwa kisingizio cha kupinga mabadiliko ya muda wa mchezo, leo Mnyama anawaalika watani zake Yanga katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Leo mchezo unapigwa saa 11 jioni, hakutakuwa na kisingizio tena, kwani hakutarajiwi kuwa na mabadiliko ya muda

Ni mechi ya ubingwa kwa Simba. Kimahesabu Simba ni bingwa anayesubiri kuapishwa lakini ushindi leo utanogesha ubingwa huo

Historia itaandikwa kuwa Julai 03, 2021 Simba ilitangaza ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo kwa kuifunga Yanga

Itabaki hivyo kwa miaka mingi, vizazi na vizazi vitasoma na kuhadithiwa historia hiyo

Ndio maana pamoja na kuwa na uhakika wa ubingwa, Simba inauhitaji sana mchezo kutengeneza rekodi juu ya rekodi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', amewahakikishia Wanamsimbazi kuwa leo ni siku ya furaha kwao akiwataka wajitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa ndani ya uzi wao mwekundu na mweupe kunogesha tukio la kihistoria linalokwenda kuandikwa

Sawa, wapo wanaosema mpira unadunda na wakati mwingine una matokeo ya kikatili, lakini jambo hili huwa ni gumu sana pale Simba inapokuwa inazihitaji alama tatu

Hapo kwa Mkapa hakuna aliyewahi kupona pale Mnyama anapoamua kuchukua alama tatu. Inakuwa sio ombi tena ni lazima, utazitoa

Wamekufa vigogo hapo msimu huu hakuna aliyetoka salama, hakuna anayetarajia jambo tofauti leo

Mashabiki wa Simba leo watafanya tukio maalum baada ya dakika 90 kukamilika, watawapigia makofi wachezaji wao kwa dakika tano baada ya ushindi dhidi ya Yanga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’