Tuko tayari kwa dabi - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jul 2021
Tuko tayari kwa dabi - Matola

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wako tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza na Wanahabari katika Mkutano maalum kuelekea mchezo huo, Matola amesema wanafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini wamefanya maandalizi sahihi ya kuwawezesha kuondoka na ushindi

Aidha Matola amesema kikosi kiko kamili, hawana mchezaji majeruhi, Jonas Mkude atakosekana kutokana na changamoto za kinidhamu wakati Ibrahim Ajibu ni mgonjwa

"Sisi tumejiandaa kikamilifu kuekea mchezo huu. Vijana wana ari na wako tayari kwa mchezo. Tunafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini tumefanya maandalizi. Tunahitaji kushinda ili tuweze kuwa mabingwa"

"Katika mchezo wa kesho tutawakosa wachezaji wawili, Ibrahim Ajibu ambaye anasumbuliwa na Malaria na Jonas Mkude suala lake halijamalizika lakini wengine wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo. Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kushinda kwa kuwa tunataka kutangazwa mabingwa baada ya mechi"

Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' kwa upande wake amesema dhamira ya kila mchezaji ni kuona wanashinda mchezo wa Jumamosi ili kuwa mabingwa kwa msimu wa nne mfululizo

"Tumejiandaa vizuri, kila mmoja anajua umuhimu wa ushindi dhidi ya Yanga, naamini kwa maandalizi tuliyofanya, tutaondoka na ushindi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’