Tangu msimu uliopita, wachezaji wa Simba wanavuna fedha kila walipofanya vizuri kwenye mechi za ndani na ligi ya mabingwa
Hizi ni fedha za bonus ambazo ziko nje ya mishahara minono wanayolipwa kila mwezi
Utamaduni huu utaendelea hata katika mchezo wa kesho dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema wameandaa fedha nyingi za bonus kwa ajili ya wachezaji kama watashinda mchezo dhidi ya Yanga
Ikumbukwe ushindi katika mchezo huu, utaihakikishia Simba kutwaa ubingwa mbele ya watani zao
"Tumekuwa tukitoa fedha za bonus kwenye kila mchezo ambao tunashinda, tumeandaa fedha nyingi kwa ajili ya ushindi wa mchezo wa Jumamosi. Siwezi kutaja ni kiasi gani lakini nikwambie ni fedha nyingi," alisema Barbara
Katika mchezo uliopaswa kupigwa May 08, inaelezwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliwaandalia wachezaji kitita cha Tsh Bilioni 300