Kapombe kuanza mazoezi wiki ijayo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Oct 2017
Kapombe kuanza mazoezi wiki ijayo
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amemuongezea wiki moja ya mapumziko beki wa pembeni wa timu hiyo, Shomari Kapombe kabla ya kurejea uwanjani kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake.

Kapombe aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Azam FC, hakufanikiwa kucheza mechi yoyote ya timu yake hiyo mpya baada ya kupata majeraha ya nyonga.

Beki huyo, alipata majeraha hayo ya nyonga akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na mechi dhidi ya Rwanda katika mechi ya marudiano kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).

Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema kwa mujibu wa ripoti ya daktari wao, Kapombe alitarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu wiki hii, lakini ameongezewa wiki moja ya kupumzika.

Ally alisema, Kapombe anatarajiwa kuanza tena mazoezi ya pamoja na wenzake wiki ijayo akiwa fiti kwa ajili ya kuichezea Simba.

Alisema kurejea kwa beki huyo kutaimarisha kikosi hicho katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ili kuhakikisha wanashinda.

Ò€œKapombe amepona na yupo fiti kabisa kwa ajili ya mapambano na alitakiwa kuanza mazoezi Jumatatu ya wiki hii, lakini ameongezewa siku za mapumziko ili akirejea awe fiti zaidi,Ò€ alisema Ally.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’