Mabingwa wa ligi kuu ya Wanawake kwa misimu miwili mfululizo, Simba Queens wamekamilisha usajili wa mlinzi wa kati Wema Richard Maile anayetokea klabu ya Mlandizi Queens
Maile anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba Queens katika kipindi cha usajili wa dirisha kubwa
Simba Queens tayari imewasajili mshambuliaji Aisha Juma Mnunka kutoka Alliance Girls na mlinzi wa Kimataifa kutoka Zimbabwe, Mwanadada Danai Bhobho


Kocha Mussa Hassan Mgosi anaendelea kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake kwa msimu wa tatu mfululizo
ADVERTISE HERE