Mwamuzi kutoka mkoani Arusha Emmanuel Mwandembwa atakuwa 'pilato' wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi Julai 03 uwanja wa Benjamin Mkapa
TFF imeweka hadharani orodha ya maafisa 14 ambao watasimamia mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni
Waamuzi watakaomsaidia Mwandemba ni Frank Komba kutoka jijini Dar es salaam na Hamdani Said kutoka mkoani Mtwara
Mwamuzi wa akiba ni Ramadhani Kayoko wakati mkaguzi wa Waamuzi ni Saoud Abdi kutoka Arusha

ADVERTISE HERE