Uchaguzi TFF umefuata sheria na taratibu - Rage

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jul 2021
Uchaguzi TFF umefuata sheria na taratibu - Rage

Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT) kwa sasa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Ismail Aden Rage, amesema mchakato wote wa uchaguzi wa shirikisho hilo, umefanyika kwa kufuata taratibu zote za sheria na kanuni, tofauti na baadhi ya watu wanavyolalamika

Rage ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba,  amesoma sheria zote za uchaguzi na kanuni zake na hajaona hata sehemu moja ambayo imepindishwa au kusiginwa

Juzi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Benjamin Kalume, alitangaza uamuzi wa kamati hiyo kumpitisha Wallace Karia anayetetea nafasi yake kwenye kiti cha Urais wa TFF akiwa mgombea pekee baada ya wagombea wawili waliobaki kwenye awamu ya pili, Hawa Mninga na Evance Mgeusa, kuenguliwa kwa vigezo vya kukosa sifa.

"Mimi nimesoma sheria na kanuni zote za uchaguzi, kamati iko sahihi kabisa. Hawajakosea, na nimeona hata wagombea wenyewe wamekiri na kukubali," Rage aliliambia Nipashe

Kiongozi huyo aliwataka watu wanaotaka kugombea uongozi kuwa wale ambao wameshawahi kucheza soka, au kuongoza klabu mbalimbali na si kila mtu tu anaweza kuongoza taasisi hiyo kubwa ya soka nchini.

"Kuongoza soka ni kazi ngumu. Sisi tumepita pale, tunajua hilo. Huwezi kutoka tu huko na kuwa kiongozi wa soka, kwa hiyo nawashauri wawe wanajipanga kweli"

Aliongeza kuwa kati ya wagombea wote ambao walijitokeza safari hii, mtu ambaye alikuwa ana uwezo wa kumtikisa Karia ni mwanasoka wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay.

"Yule alikuwa na uwezo wa kuongoza, lakini kwa bahati mbaya alishindwa mwanzoni. Na Kamati ilikuwa sawa tu tangu mwanzoni, kwani ilikuwa ikifanya hivyo kutokana na kanuni zilizopitishwa na wajumbe wenyewe"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’