TFF watuletee kombe letu kwa Mkapa - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jun 2021
TFF watuletee kombe letu kwa Mkapa - Manara

Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano klabu ya Simba,Haji Manara amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza na Wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Manara amesema utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani lakini wana matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi

"Tuko tayari, dhamira yetu ni matokeo, kuwapa watu furaha. Wanasimba wanataka ushindi, bila shaka tutashinda na kuwa mabingwa"

"Simba ndio timu bora kuwahi kutokea Afrika Mashariki kupata matokeo mazuri.”

"Heshima ya mpinzani lazima iwepo kama ambavyo huwa tukicheza na timu zingine. Mechi itakuwa nzuri"

"Hii ni mechi kubwa, tunahitaji mashabiki waje kwa wingi. Nawaomba Wanasimba baada ya mchezo tukiwa tumeshinda tubaki uwanjani na tuwapigie makofi wachezaji wetu kwa dakika tano kwa kuwa mabingwa mara nne mfululizo," alisema Manara

Aidha Manara amesema wamepeleka ombi kwa TFF waweke kombe uwanjani ili kama watashinda mchezo huo wakabidhiwe ubingwa wao

"Niwaombe TFF kama itawapendeza watuletee kombe pale"

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Julai 03 kuanzia saa 11 jioni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
55m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’