Hawa akina Chama mpira uko damuni mwao! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mlinzi wa Zesco United Adrian Chama kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Zambia msimu huu
Adrian ni kaka wa kiungo wa Simba Clatous Chama ambaye amerejea hivi karibuni kutoka Zambia baada ya kumaliza msiba wa mkewe
Ndugu hawa wawili wamekuwa na historia ya maisha ya soka inayovutia sana
Wote ni wachezaji wa timu ya Taifa na wachezaji tegemeo katika klabu zao
Clatous yeye aliibuka kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita, msimu huu nduguye ni kama 'amemlipa'
Clatous amekuwa na msimu mzuri sana na Simba mpaka sasa akiwa kinara wa pasi za mabao (13). Pengine anaweza kushinda tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa pili
Kuna wakati Adrian alihusishwa kutakiwa na Simba, inaelezwa mpango huo bado upo
Hawa ni ndugu wawili ambao wanapokuwa uwanjani kwa hakika wanavutia kuwatizama vile wanavyolisakata gozi la ng'ombe