Jana Kaizer Chiefs walifanikiwa kutinga fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla wa bao 1-0 dhidi ya Wydad Athletic
Chiefs waliifunga Wydad bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Morocco
Aidha Al Ahly wametinga fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-0 dhidi ya Esperance
Walishinda bao 1-0 ugenini na jana kushinda mabao 3-0 nyumbani
Kwa hakika huu ulikuwa msimu wa Simba kucheza fainali ya ligi ya mabingwa na pengine hata kutwaa ubingwa
Timu zote zilizotinga fainali zilichezea vichapo dhidi ya Simba
Zaidi ni Kaizer Chiefs ambao kwa hakika walikuwa na bahati kwelikweli kutinga nusu fainali mbele ya Simba
Bila shaka msimu ujao yale yaliyojitokeza msimu huu yatarekebishwa ili kuhakikisha Simba inavuka robo fainali