Ndivyo wanavyotamba mashabiki wa Simba baada ya kuishuhudia timu yao ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc na kutinga fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Jambo la kufurahisha zaidi ni kuwa Mnyama anakutana na mtani wake Yanga katika mchezo wa fainali utakaopigwa mkoani Kigoma Julai 25
Simba inaweza kushinda mataji matatu kupitia mgongo wa Yanga katika kipindi cha miezi miwili
Julai 03 timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa duru ya pili ligi kuu ya Vodacom mchezo ambao kama Simba itashinda basi itatwaa rasmi ubingwa wa ligi kuu
Aidha, ushindi katika mchezo wa Julai 25 utamshuhudia Mnyama akitwaa kombe la Shirikisho (FA)
Mchezo wa ufunguzi wa msimu ujao (Ngao ya Jamii) utawakutanisha tena ambapo Mnyama anaweza kuanza msimu 2021/22 na Ngao ya nne!
Hapa hakuna kukimbia tena...!