Mabingwa watetezi michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Simba wametinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majimaji, Songea
Ulikuwa mchezo mgumu uliowahitaji wachezaji kama Bernard Morrison kuweza kuisaidia Simba kupata ushindi
Morrison ndiye aliyebadili taswira ya mchezo baada ya kuingia kwenye kipindi cha pili
Ilikuwa dakika ya 88 alifanyiwa madhambi nje kidogo ya 18. Akaanzisha mpira wa adhabu kwa haraka kumuwekea Luis Miquissone aliyeweka mpira wavuni
Azam Fc hawakuamini kilichotokea lakini kwa Mnyama zilisikika nderemo za mashabiki wake walioujaza uwanja wa Majimaji
Simba sasa imetinga fainali na itachuana na mtani wake Yanga katika mchezo unaotarajiwa kupigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
Hakika zitakuwa dakika 180 za wachezaji wa Simba kuonyesha ukubwa wao dhidi ya wenzao wa Yanga
Kinaanza kupigwa Julai 03 halafu mwishoni mwa mwezi Julai 25 kinapigwa tena...!