Ingekuwa enzi zetu tungewachezesha waarabu mchana - Rage

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
8 Mar 2018
Ingekuwa enzi zetu tungewachezesha waarabu mchana - Rage
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismali Aden Rage amesema Simba ingeweza kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry kama mchezo huo ungechezwa mapema.

Mchezo huo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa ulianza saa 12:00 jioni na ulimalizika kwa matokeo ya sare ya 2-2.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Rage amesema anaamini Simba ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa kama mchezo huo ungechezwa saa 8:30 au saa 9:00 mchana.

Rage amesema zamani waliitumia mbinu hiyo ya kuwachezesha waarabu mchana wa jua kali hivyo kuwafunga kwa urahisi.

“Bado nasikitika sana kwa jinsi nilivyoona Simba wamecheza vizuri, kama mpira ungechezwa saa 8:30 au saa 9:00 mchana wale waarabu walikuwa wepesi sana leo kwetu," amesema Rage.

"Hizo ndio mbinu za mpira lazima ufanye mambo kwa kuangalia utafaidika vipi, huko nyuma tumewahi kushinda michezo mingi dhidi ya waarabu tunapocheza saa 8:30 au saa 9:00.”

“Nasema hivyo kwa sababu hali ya hewa ya Cairo sasa hivi ni nyuzi joto kati ya 7 hadi 8 na kwa vyovyote vile itakavyokuwa, sisi watatuchezesha usiku ambapo hali ya hewa itakuwa ni nyuzi joto 7 ambayo itatuathiri kidogo kwa sababu kutakuwa na ubaridi ambao hatujauzoea labda tuende mapema zaidi.”

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa nchini Misri, March 16. Katika mchezo huo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili iweze kufuzu
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →