Mabingwa wa nchi Simba ambao ni watetezi kombe la FA wamekamilisha maandalizi yao ya mwisho kuelekea mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma
Vijana wa kocha Didier Gomes wako tayari kuwapa furaha Wanamsimbazi siku ya kesho
Simba inahitaji kuifunga Azam Fc ili kujihakikishia kutinga fainali ambayo watakutana na watani zao Yanga
Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ulipigwa jioni ya leo na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United
Walikimbia May 08 lakini sasa hawatakuwa na pa kutokea. Wakati Julai 03 inawasubiri, dabi nyingine inaweza kwenda kupigwa Kigoma
ADVERTISE HERE