Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji 'Mo' anajitolea fedha nyingi kuiendesha Simba
Barbara amesema pamoja na mafanikio ambayo Simba inaonekana kuyapata, lakini bado haijaweza kujiendesha yenyewe
"Simba hatujiendeshi kwa faida, nitakuwa muongo kama nikisema tunajitegemea wenyewe na kuwa kila kitu kiko sawa"
"Mo anajitolea fedha nyingi sana. Bila Mo tusingeweza kulipa mishahara ya wachezaji, bila ya Mo pengine tusingeweza kulipa bonus ," alisema Barbara
"Najua hili sio tatizo la Simba tu, ukiangalia mpira wa Ulaya kwa mfano, timu nyingi ziko katika wimbi kubwa la madeni, timu haziendeshwi kwa faida"
Pamoja na kuwa Mwekezaji ndani ya klabu ya Simba, Mo amejipambanua kwa kuwa Mwanasimba kwelikweli
Mwezi uliopita baada ya Simba kutolewa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, Bilionea huyo aliachana na mpango wa kujizawadia magari ya kifahari na kuwekeza fedha hizo katika kuiimarisha Simba