Simba inaendelea na maandalizi yake Songea kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majimaji
Wababe hao wa soka la Tanzania, wamepania kulirejesha kombe la FA pale viunga vya Msimbazi kwa msimu wa pili mfululizo
Wakati mwingine Azam Fc wanakuwa wabishi wanapokutana na Simba, lakini kiungo Mzamiru Yassin amesema wanachofahamu watashinda na kutinga fainali
Mzamiru maarufu 'kiungo punda', amesema ubora wao unawapa sababu ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Azam
"Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Azam ni timu nzuri na inatupa ushindani mkubwa lakini tumejipanga kuwakabili na lengo letu ni moja kuingia fainali na tutapambana kuhakikisha tunafanikisha," alisema Mzamiru
SImba imepania kushinda mataji yote ya ndani kama walivyofanya msimu uliopita
Mwanzoni mwa msimu walishinda Ngao ya Jamii, tayari wanahesabu siku kutangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu na kesho Jumamosi wamepania kuingia fainali ya FA