Wachezaji wasiojitambua watahadharishwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Jun 2021
Wachezaji wasiojitambua watahadharishwa Simba

Juzi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez alitahadharisha kuwa klabu haitakuwa tayari kuendelea na wachezaji ambao hawana kiu ya mafanikio na kuipambania timu

Kauli hiyo pia ikakolezwa na Mulamu Ng'ambi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye amesema kwa sasa Simba haihitaji wachezaji wa mshahara tu

Ng'ambi alisema Simba ina maono makubwa hivyo inahitaji wachezaji wenye maono makubwa pia

Mabosi wa Simba ni kama wanawaandaa 'kisaikolojia' baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa na mchango mdogo ndani ya kikosi cha Simba

Kuna panga litapita msimu utakapomalizika, kwa nyota ambao wamekuwa na msaada mdogo katika timu

Aidha suala la nidhamu pia huenda likawaingiza matatani nyota kama Gerard Mkude ambaye bado anaendelea kuvutana na uongozi licha ya kuwa zinafanyika jitihada kumsaidia nyota huyo aliyedumu zaidi kwenye kikosi cha Simba

Simba inalenga kufanya vizuri zaidi msimu ujao hasa kwenye michuano ya Kimataifa

Pamoja na kuwa Kocha Didier Gomes hahitaji mabadiliko makubwa ya kikosi chake, lakini ni wazi baadhi ya wachezaji wataachwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’