Jana Simba iliweka historia mkoani Ruvuma kwa kupata mapokezi ya aina yake kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc
Umati wa mashabiki waliojitokeza kuwalaki mabingwa hao wa nchi mjini Songea, umeweka rekodi
Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola, amewashukuru Wanasimba kuwapa mapokezi ya kipekee huku akiahidi kuwapa furaha Jumamosi
"Tunawashukuru Wanasimba wa Ruvuma, kwa kweli wametupa mapokezi ya kipekee. Tunawashukuru kwa kutuunga mkono na tunawaambia waje kwa wingi uwanjani siku ya Jumamosi"
"Tumekuja hapa tukiwa na karibu wachezaji wote, tunahitaji kushinda mchezo dhidi ya Azam, tuna malengo ya kutetea taji la FA, naamini tutafanikiwa," alisema Matola
Baada ya kutua Ruvuma jana mchana,Simba ilifanya mazoezi yake ya kwanza jioni ambapo kocha Matola amesema hali ya hewa ya Ruvuma ni nzuri

"Hali ya hewa ni nzuri hapa, tuna siku nne za kujiandaa kabla ya mchezo wenyewe. Naamini kila kitu kitakuwa sawa"