Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City hapo jana, mabingwa wa nchi Simba wamebakisha alama tatu tu, kushangilia ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Simba sasa inahamishia nguvu zake kwenye michuano ya kombe la FA, ambapo inaelekea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc
Mchezo dhidi ya Azam Fc utapigwa Jumamosi, Juni 26, uwanja wa Majimaji
Baada ya kukosa burudani ya ligi kuu kwa takribani misimu mitatu, Mnyama anawapelekea burudani watu wa Ruvuma
Huku ndiko alikozaliwa kiraka Erasto Nyoni ambaye amewaahidi tiketi 50 mashabiki wa Simba hapo Songea
Simba imedhamiria kubakisha mataji yake yote waliyoshinda msimu uliopita
ADVERTISE HERE