Ni suala la muda tu Simba itarudisha kabatini ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Kikosi cha kocha Didier Gomes kina ubora 'uliopitiliza'! Sio rahisi kwa klabu za hapa Tanzania kuweza kushindana na mnyama!
Usemi huu utaenda kuthibitika tena hii leo pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati vijana wa Gomes watakapoikaribisha Mbeya City
Ni mchezo ambao Simba inafukuzia kukamilisha hesabu zake za ubingwa mapema, alama tatu ndio hesabu ya mabingwa hao wa nchi
Wanakutana na Mbeya City ambayo bado haijaondoka kwenye presha ya kushuka daraja
Ni bahati mbaya sana kwao kukutana na 'Mnyama' wakati huu kwani Wanamsimbazi wana jambo lao Julai 03
Julai 03 kutakuwa na sherehe pale uwanja wa Benjamin Mkapa, watu wanataka kushangilia ushindi dhidi ya Yanga na ubingwa!
Jana kiungo fundi, kinara wa pasi za mabao Clatous Chama alirejea baada ya kukosekana kwa takribani wiki tatu kutokana na msiba wa kufiwa na mkewe
Chama amenyesha yuko tayari pengine Gomes leo anaweza kumpa nafasi kulingana na mahitaji ya kikosi chake
Mchezo utaunguruma kuanzia saa moja kamili usiku..