Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesisitiza kuwa hatarajii kufanya usajili wa wachezaji wengi wa ndani kwani tayari anao wazuri katika kikosi chake
Gomes amedokeza kuwa nyota wapya atakaowasajili hawatazidi watatu na inawezekana wakatoka nje ya nchi
Simba imekuwa ikihusishwa na wachezaji kadhaa wa ndani hivi karibuni ikidaiwa kumsajili mlinzi wa kushoto Edward Charles Manyama ambaye hata hivyo siku moja baadae ikatangazwa kuwa amesajiliwa na Azam Fc
Gomes amesema kikosi chake kimejitosheleza kwa wachezaji wa ndani, kwa sasa anaangalia maboresho kwa ajili ya mechi za Kimataifa
Hata hivyo kocha huyo raia wa Ufaransa amesema atawasilisha ripoti yake kwa mabosi baada ya msimu kumalizika
"Usajili wa wachezaji wandani nadhani si uhitaji mkubwa kwetu kwani ambao nipo nao katika timu ni bora mno na nimewaeleza nahitaji kuwa nao zaidi lakini kama kuna ambaye atapata maslahi mengine anaweza kwenda nampa ruhusa na nafasi yake tutaongeza"
"Wachezaji wa nje ya nchi, ndio tutasajili kwani kuna hitaji hilo, lakini tuliache kwanza hili muda ukifika nitalieleza kwa upana kwani sasa akili ni kuchukua ubingwa wa ligi pamoja na kombe na Shirikisho (ASFC)," alisema Gomes