Gomes apania kutangaza ubingwa Julai 03

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jun 2021
Gomes apania kutangaza ubingwa Julai 03

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kikosi chake kimepania kutangaza ubingwa Julai 03 kwenye mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania hapo jana, Simba inahitaji kushinda mechi mbili tu ili kutangaza ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

Keshokutwa Jumanne mabingwa hao wa nchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo ambao kama watashinda, basi watahitaji alama nyingine tatu kutangaza ubingwa

Alama hizo wanazo Yanga! kwani mchezo wa ligi utakaofuata ni dhidi yao Julai 03

"Tumedhamiria kupata ushindi mchezo dhidi ya Yanga. Hii ni mechi muhimu ambayo inaweka rekodi kubwa kwetu kwa kuhakikisha ubingwa umerejea nyumbani tena, katika mchezo mkubwa na ninaamini hilo linawezekana," alisema Gomes

"Tunahitaji kushinda mechi mbili zijazo, baada ya ushindi dhidi ya Polisi Tanzania tunarudi Dar es Salaam kuishughulikia Mbeya City, baada ya hapo ndipo tutakutana na Yanga, itakuwa nzuri kushinda kombe mbele yao, nitakuwa mtu mwenye furaha kwa mafanikio hayo"

Aidha Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema haoni timu ya kuizuia Simba isiweze kushinda mechi zilizobaki ili kutangaza ubingwa mapema

"Kabla ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, tulifahamu kuwa tunahitaji kushinda mechi zetu tatu zijazo ili kuwa mabingwa. Tunapambana kufanikisha hilo na kwa hakika hakuna kitakachotuzuia," alisema Matola

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’