FT : Simba 2-2 Al Masry

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Mar 2018
FT : Simba 2-2 Al Masry
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba wamelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Al Masry kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho, mzunguuko wa kwanza.

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa ulikumbwa na matukio ya hapa na pale yakiwemo mabao matatu ya mikwaju ya penati na tukio la Umeme kukatika kwa zaidi ya dakika 15 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es salaam.

Simba ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya tisa kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na nahodha John Bocco.

Beki wa Al Masry Koffi aliunawa mpira wa kichwa uliopigwa na Bocco ambao ulikuwa unaelekea wavuni.

Al Masry walisawazisha dakika mbili baadae kupitia kwa Ahmed Gomaa na wakapachika bao la pili kwenye dakika ya 26 kupitia mkwaju wa penati wa Ahmed Abdallarof baada James Kotei kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Kipindi cha pili Simba iliingia kwa kasi kusaka bao la kusawazisha na la ushindi.

Juhudi za wachezaji wa Simba zilizaa matunda kwenye dakika ya 74 baada ya Emanuel Okwi kuwapangua walinzi wa Al Masry ndani ya eneo la hatari kabla mlinzi yuleyule aliyesababisha penati ya kwanza, Koffie kuunawa tena mpira.



Okwi aliisawazishia Simba kupitia mkwaju huo wa penati.

Wakati Simba ikiwa imechanganya kusaka bao la ushindi ghafla umeme ulikatika na kusababisha giza totoro uwanjani kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

Hata umeme uliporejea hali ya uwanja haikuwa rafiki kwani uwanja ulijaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

Mpambano huo ukafika mwisho kwa sare ya mabao 2-2.

Sasa Simba ina kazi ya ziada ya kuibuka na ushindi ugenini wakati timu hizo zitakaporudiana nchini Misri March 16.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’