Tuko tayari kuikabili Polisi Tanzania - Matola

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jun 2021
Tuko tayari kuikabili Polisi Tanzania - Matola

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuweza kupata ushindi dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba

Akizungumza kwenye Mkutano maalum wa mchezo, Matola amesema wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi saa kumi Alasiri

Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kuharakisha mpango wa kushinda ubingwa wakifahamu wanahitaji kushinda michezo mitatu tu

"Kikosi kipo kamili wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunawaheshimu Polisi mara zote tukikutana wanatupa ushindani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda

"Tumewafunga katika mechi zote tatu za ligi tulizokutana nao, mbili za msimu uliopita na moja msimu huu lakini haimaanishi mechi ya kesho itakuwa rahisi kwetu, tutaingia kwa tahadhari na lengo letu ni kushinda ili kusogelea ubingwa wa ligi," alisema Matola

Naye nahodha msaidizi Mohamed Hussein, amesema kila mchezaji anafahamu umuhimu wa ushindi katika mchezo huo kuelekea ubingwa wa nne mfululizo

"Sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu na lengo la kila mmoja ni kuhakikisha tunashinda ili kutetea ubingwa hivyo yeyote atakayepewa nafasi atafanya hivyo," alisema Tshabalala

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’