Kikosi cha timu ya vijana U20 jana kimeondoshwa kwenye michuano ya ligi kuu ya vijana kwa kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar
Nadhani uongozi wa Simba unapaswa kutilia mkazo kikosi hiki kwa kufanya maboresho kwani huu ni msimu wa tatu Simba U20 inashindwa kutamba kwenye michuano hiyo
Aidha kwa hadhi ya Simba sasa, timu ya vijana haiendani na vile Simba ilivyo
Timu haina ubora ukilinganisha na timu ya wakubwa na ile ya kinadada
Bila shaka michuano ya msimu ujao, uongozi utachukua hatua kwa kufanya maboresho muhimu ili vijana waweze kufanya vizuri
ADVERTISE HERE