Kocha Simba anaamini Bocco ataibuka mfungaji bora VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jun 2021
Kocha Simba anaamini Bocco ataibuka mfungaji bora VPL

Kasi ya kufunga mabao aliyonayo mshambuliaji na nahodha wa kikosi cha Simba, John Bocco imemuibua kocha wake Mtunisia, Adel Zrane ambaye amesema ana imani kubwa mshambuliaji huyo ndiye atakayeibuka na tuzo ya ufungaji bora msimu huu

Bocco ambaye Jumapili iliyopita alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata Taifa Stars kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi, amekuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Simba

Mpaka sasa ameifungia Simba mabao 13 yanayomuweka katika nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora msimu huu nyuma ya Prince Dube wa Azam mwenye mabao 14

Mshambuliaji huyo amefunga mabao saba katika michezo minne mfululizo iliyopita ya michuano mbalimbali, aliyoshuka uwanjani kuichezea Simba na timu ya Taifa Stars

Zrane amesema Bocco ana nafasi kubwa ya kuibuka na tuzo ya mfungaji bora kama ataendeleza makali aliyonayo sasa

"Vita ya ufungaji bora msimu huu inaonekana kuwa na ushindani mkubwa sana, misimu miwili iliyopita mshambuliaji wetu, Meddie Kagere alitwaa tuzo hiyo mfululizo, lakini msimu huu tayari Dube wa Azam, na Bocco wameongezeka kwenye huo ushindani"

"Lakini licha ya kasi aliyonayo Dube mwenye mabao 14, nakuhakikishia kuwa mfungaji bora wa msimu huu atakuwa Bocco kwa kuwa ana kila sababu ya kufanya hivyo, zaidi ya hiyo nina uhakika kuwa Dube atamaliza katika nafasi ya tatu kwani mfungaji bora namba moja na yule wa pili wa ligi watatoka ndani ya kikosi cha Simba," Zrane alinukuliwa na Championi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’