Pamoja na kutokuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, winga Miraji Athumani amepewa ofa ya kuhuisha mkataba wake na mabingwa wa soka Tanzania, Simba Sc
Benchi la ufundi la Simba limependekeza nyota huyo aongezwe mkataba baada ya mkataba wake wa awali kumalizika
Miraji alitua Simba mwaka juzi akitokea klabu ya Lipuli Fc
Alianza maisha yake vizuri lakini majeraha aliyopata mwaka uliopita na kumuweka nje kwa zaidi ya miezi nane, yalipunguza kasi yake
Kwa sasa Miraji yuko timamu kiafya, kitendo cha benchi la ufundi kupendekeza aendelee kubaki, inaamisha bado anahitajika
Msimu huu Simba haitarajii kufanya usajili mkubwa wa wachezaji wa ndani, kocha Didier Gomes akitaja sababu kuwa hakuna wachezaji wazuri zaidi ya wale alionao licha ya kuwa wengine hawapati nafasi kutokana na ushindani uliopo