Mabingwa wa nchi Simba tayari wamewasili jijini Mwanza kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Jumamosi Juni 19 uwanja wa CCM Kirumba
Simba imetua Mwanza ikiwa na kikosi chake kamili, wachezaji watatu tu Clatous Chama, Ibrahim Ajibu na Jonas Mkude ndio wanaokosekana kutokana na sababu mbalimbali
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema timu imeingia mapema Mwanza ili kupata muda wa kutosha kufanya maandalizi
Rweyemamu amesema wachezaji wengi walikuwa na majukumu ya timu za Taifa, hivyo watapata angalau siku tatu za kufanya mazoezi ya pamoja kabla ya mchezo huo



ADVERTISE HERE