Leo Simba inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Al Masry katika mchezo wa kombe la Shirikisho raundi ya kwanza.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:00 jioni kuwapa nafasi mashabiki wengi kuweza kuushuhudia.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre alisema anawafahamu vyema wapinzani wao kutoka Misri hivyo ameahidi Simba kuibuka na ushindi.
Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika amesema Simba imejiandaa kikamilifu na haoni sababu ya kutofanya vizuri kwenye mchezo huo wa kwanza unaopigwa nyumbani.
Simba SC imekuwa kambini katika hoteli ya Sea Scape Kunduchi, Dar es Salaam ikifanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani.
Al Masry wapo Dar es Salaam tangu Jumamosi na wamefikia katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski huku wakifanya mazoezi Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam.
Simba ndiyo timu pekee kutoka Tanzania ambayo imekuwa na rekodi ya kuridhisha dhidi ya timu kutoka nchi za Waarabu.
Na ndio sababu mashabiki wengi wana matumaini makubwa kwa Simba kuibuka na ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa kuwa imekuwa ikifanya hivyo mara nyingi dhidi ya timu kutoka Misri.

ADVERTISE HERE