Mkude anachezea shilingi chooni

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Jun 2021
Mkude anachezea shilingi chooni

Kiungo Jonas Mkude anaweza kuwa matatani kama ataendelea kukaidi maagizo anayopewa na uongozi

Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba inayoongozwa na Kamanda mstaafu, Suleiman Kova ilipendekeza Mkude kufanyiwa vipimo  vya afya Hospitalini kutokana na kujirudia kwa makosa anayofanya mara kwa mara

Inaelezwa jambo hilo limekuwa gumu kwa Mkude, sasa kitakachomnusuru ni huruma ya mabosi wa Simba tu

Akiwa mchezaji mwandamizi zaidi katika kikosi cha Simba, ukweli ni kuwa mchango wake umethaminiwa sana na Simba na ndio maana uongozi umejaribu kufanya jitihada za kumsaidia ili aondokane na changamoto zinazomuingiza matatani kila mara

Ni nadra sana timu kumvumilia mchezaji anayevunja kanuni na taratibu za klabu kila mara, lakini Mkude amevumiliwa na kupewa nafasi nyingine kila wakati

Mkude ni mchezaji aliyeitumikia Simba kwa zaidi ya miaka 10, yeye binafsi alipaswa kutambua hili na kujiepusha na matukio ya utovu wa nidhamu

Alipaswa kuwa nahodha wa Simba kutokana na ukongwe wake kikosini lakini badala yake amekuwa mchezaji mwenye mvutano zaidi na uongozi

Pamoja na kuwa bado ana mkataba na Simba, yuko hatarini kuonyeshwa mlango wa kutokea

Naamini hii ni nafasi ya mwisho kwake, akiipoteza, Simba haitamvumilia zaidi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
34m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’