Kiungo Jonas Mkude anaweza kuwa matatani kama ataendelea kukaidi maagizo anayopewa na uongozi
Hivi karibuni Kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba inayoongozwa na Kamanda mstaafu, Suleiman Kova ilipendekeza Mkude kufanyiwa vipimo vya afya Hospitalini kutokana na kujirudia kwa makosa anayofanya mara kwa mara
Inaelezwa jambo hilo limekuwa gumu kwa Mkude, sasa kitakachomnusuru ni huruma ya mabosi wa Simba tu
Akiwa mchezaji mwandamizi zaidi katika kikosi cha Simba, ukweli ni kuwa mchango wake umethaminiwa sana na Simba na ndio maana uongozi umejaribu kufanya jitihada za kumsaidia ili aondokane na changamoto zinazomuingiza matatani kila mara
Ni nadra sana timu kumvumilia mchezaji anayevunja kanuni na taratibu za klabu kila mara, lakini Mkude amevumiliwa na kupewa nafasi nyingine kila wakati
Mkude ni mchezaji aliyeitumikia Simba kwa zaidi ya miaka 10, yeye binafsi alipaswa kutambua hili na kujiepusha na matukio ya utovu wa nidhamu
Alipaswa kuwa nahodha wa Simba kutokana na ukongwe wake kikosini lakini badala yake amekuwa mchezaji mwenye mvutano zaidi na uongozi
Pamoja na kuwa bado ana mkataba na Simba, yuko hatarini kuonyeshwa mlango wa kutokea
Naamini hii ni nafasi ya mwisho kwake, akiipoteza, Simba haitamvumilia zaidi