Baada ya mapumziko ya wikiendi, mabingwa wa nchi Simba leo wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Polisi Tanzania
Mchezo huo utapigwa Juni 19 mkoani Mwanza uwanja wa CCM Kirumba
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes tayari amerejea kuendelea na majukumu yake baada ya kumaliza mapumziko yake nchini Ufaransa
Aidha kwa wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa, Patrick Rweyemamu, meneja wa Simba amesema wanatarajia kuanza kuwapokea leo kambini
Kimahesabu Simba inahitaji kushinda michezo mitatu tu kuweza kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo
Mechi saba zimesalia kwa mabingwa hao wa nchi, ni muujiza pekee ambao utawafanya wakose ubingwa
ADVERTISE HERE