Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kim Poulsen amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na wako tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Poulsen amesema wanafahamu wanakwenda kukutana na timu ambayo iko juu yao katika viwango lakini wamefanya maandalizi mazuri kuweza kushinda mchezo huo
"Malawi ni timu nzuri na ipo kwenye kiwango bora na tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuonyesha kiwango safi pia. Tumefanya mazoezi kwa siku tisa uwanjani na darasani ninaimani tutacheza vizuri," alisema
Aidha, nahodha wa Stars John Bocco amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo huku akiwaita mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti